Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwamba huyu hapa! Kramo sasa yuko fiti asilimia 100

Kramo Fiti(2) Aubin Kramo.

Thu, 14 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Simba, Aubin Kramo Kouamé (27) raia wa Cote d'Ivoire amepona majeraha yake na sasa yupo tayari kwa ajili ya kuwatumikia Wekundu wa Msimbazi.

Kramo ambaye hajacheza mchezo hata mmoja wa kimashindano tangu asajiliwe na Simba mwanzoni mwa msimu huu, amekuwa akipata majeraha ya mara kwa mara jambo ambalo lilimlazimu kupewa ruhusa ndefu kwenda Tunisia kwa ajili ya matibabu ambako amemaliza takribani miezi miwili.

Chanzo cha habari hii kutoka Cote d'Ivoire kimeeleza kuwa Kramo amepona majeraha yake kwa asilimia 100 na ameanza mazoezi yake binafsi kujiweka sawa kabla ya kurejea Simba.

Chanzo hicho kimedokeza pia kuwa, fundi huyo wa boli wa zamani wa ASEC Mimosas anatarajiwa kukwea pipa wiki ijayo kuungana na wenzake ambao wanaendelea na michuano ya Ligi Kuu pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ujio wa Kramo utamfanya Kocha Benchika apate nafuu katika eneo lake la ushambuliaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live