Wakati tukifurahia timu zetu za Simba na Yanga kutinga hatua ya robo fainali ya michuono ya Ligi ya Mabingwa Afrika na ile ya Kombe la Shirikisho, mwamba huyu anapaswa kupewa heshima yake.
Uamuzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wa kuruhusu klabu zetu kusajili wacheji wengi wa kimataifa tofauti na ilivyokuwa huko nyuma ndiyo kitu pekee ambacho leo hii kimetufanya kuandika rekodi hii.
Kitendo cha kuwa na wachezaji wengi wa kigeni katika timu hizo na wenye viwango bora ndiyo chanzo kikubwa cha mafanikio haya.
Wapo baadhi ya wadau wa soka, walipinga uamuzi huo, wakidai kuwa wachezaji wazawa hawatapata nafasi ya kucheza katika timu zao jambo ambalo linaweza kusababisha tusiwe na timu bora ya taifa.
Hata hivyo, leo hii naamini watakuwa wanafurahia mafanikio ya soka letu ambalo yamefanikiwa kuyafikia.
Ngoja niishie hapa kwa leo, ila Big up sana Rais wa TFF, Wallace Karia na viongozi wako kwa kulitoa soka letu sehemu moja na kulipeleka mbele.