Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwamba anakwenda kwenye tuzo na tuzo yake mkononi

Aziz Ki Mwe Mwamba anakwenda kwenye tuzo na tuzo yake mkononi

Thu, 1 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwamba Aziz Ki ndani ya msimu wa 2023/24 alifunga jumla ya mabao 21 katika Ligi Kuu Bara ndani ya uwanja akiwa na tuzo yake mkononi kwa sasa ambayo ni ile ya mfungaji bora.

Ki ni namba moja kwa watupiaji wa mabao ndani ya ligi alipofunga jumla ya mabao 21 kati ya 71 na alitoa pasi 8 za mabao ndani ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.

Rekodi zinaonyesha kuwa alifunga mabao 17 kwa mguu wa kushoto, mabao matatu kwa mguu wa kulia na pigo la kichwa ilikuwa bao moja dhidi ya Tabora United uliochezwa Uwanja wa Mkapa alipofikisha mabao 18.

Akiwa ndani ya 18 ni mabao 15 alifunga nje ya 18 alifunga mabao 6 ambapo kwenye mabao hayo alikuwa ni mkali wa kutupia kwa mapigo huru huku mguu wake wenye nguvu ukiwa ni ule wa kushoto.

Usiku wa Tuzo 2023/24 unatarajiwa kuwa leo Agosti Mosi 2024, Masaki ambapo tuzo zitatolewa kwa wachezaji pamoja na viongozi ikiwa ni mwanzo wa kuelekea msimu mpya wa 2024/25.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: