Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwamba amerejea, Simba wajipange

Emam Ashour Sd Emam Ashour.

Thu, 21 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Fundi wa mpira ukisikia Football is Art basi Emam Ashour ni Artist anajua boli balaa mzaliwa wa pale Misri anacheza eneo la kiungo wa kati kwa ubora mkubwa kabisa.

Kwenye kikosi cha miamba ya soka Afrika, Al Ahly miongoni mwa nyota wakuchungwa basi ni Emam Ashour.

Kwenye AFCON pale Ivory Coast aliubonda balaa licha ya kukosekana kwenye baadhi ya michezo kutokana na majeraha lakini uwepo wake ulikuwa na faida katika kikosi cha Mafarao.

Kwa sasa pale Al Ahly ana mchango mkubwa kwenye kikosi cha Kocha Marcel Koller. Emam Ashour naye atakuwepo kwenye mchezo wa robo fainali ya CAF champions league Simba dhidi ya Al Ahly akiumana na wakina babacar Sarr na Fabrice Ngoma. Mchezaji wa kuchungwa kwenye hii mechi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live