Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwamba aliyewatikisa Al Ahly ndani ya Yanga

Pacomeeee Auchooo Mwamba aliyewatikisa Al Ahly ndani ya Yanga

Fri, 2 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi Al Ahly Waarabu wa Misri walikuwa ni imara kwenye upande wa ulinzi kutokana na ukuta wao kutoruhusu mabao mengi ya kufungwa katika mechi za ushindani.

Rekodi zinaonyesha kuwa mabingwa hao ambao walimenyana na Simba kwenye hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika walifugwa bao moja pekee katika hatua ya makundi.

Ikumbukwe kwamba mtupiaji alikuwa ni Pacome Zouzoua kwa shuti akiwa nje kidogo ya 18 kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Pacome bao hilo lilitajwa kuwa bao bora la wiki kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika alikuwa anatajwa kuwa miongoni mwa nyota ambao wangekuwa kwenye changamoto mpya msimu wa 2024/25 baada ya kuwatikisa Al Ahly lakini bado yupo ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.

Kwenye ligi alicheza mechi 21 akitupia mabao 7 na pasi 3 za mabao msimu wa 2023/24 na Yanga ilitwaa taji la ligi safu ya ushambuliaji ilifunga mabao 71 ikiwa namba moja kwa timu zilizofunga mabao mengi zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: