Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwalimu ndio siri ya kudaka penalti za Singida FG - Ally Salim

Ally Salim Noti.jpeg Mwalimu ndio siri ya kudaka penalti za Singida FG - Ally Salim

Thu, 11 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Golikipa wa Simba SC, Ally Salim amesema kilichomfanya aweze kuchomoa mikwaju ya penalti ya Singida FG ni maelekezo ya mwalimu wake.

Ally alisema Singida walifahamu kuwa anawajua jinsi wanavyopiga lakini yeye alizingatia vile alivyoelekezwa na mwalimu.

"Alinipa maelekezo kwamba fanya hivi fanya hivi, wakipiga fanya hivi na hivi na kweli nikafanikiwa," alisema Ally.

Kwenye mikwaju hiyo mitano iliyoelekezwa langoni kwake, Ally alifanikiwa kuchomoa mitatu kitendo ambacho kiliwafanya wapate ushindi katika mchezo huo wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya wachezaji wa Simba kufanikiwa kushinda penalti 3 kati ya nne walizopiga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live