Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwakalebela ang'atuka Yanga, amuunga mkono Eng. Hersi urais

Inj Hersi Said M.jpeg Engineer Hersi Said

Thu, 9 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Frederick Lugano Mwakalebela amewaaga rasmi wanachama wa Yanga SC kwamba hatokuwa tena kwenye nafasi za juu ndani ya klabu hiyo.

Mwakalebela aliyefanya kazi chini ya Mwenyekiti, Dkt. Mshindo Msola ametangaza wazi sifa lukuki za Mhandisi Hersi Said kuwa anafaa kuchaguliwa na Wanayanga kuwa rais wa klabu hiyo ambaye hiyo.

"Sikuwa na mpango wa kugombea katika uchaguzi huu, pia sikutaka kuwaacha bure Wanayanga hivyo nimeamuo kumsaidia Eng.Hersi kwa sababu naiona dhamira yake njema kwa wana Yanga," amesems Mwakalebela.

Hersi hii leo amerudisha fomu yake iliyowasilishwa na Mzee Mohamed Msumi katika ofisi za makao makuu klabu hiyo, Jangwani jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa Yanga, Malangwe.A. Mchungahela amesema kuwa Uchaguzi Mkuu utafanyika tarehe 10/7/2022 jijini Dar es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live