Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwakalebela: Robertinho ni Comedy, Ningekuwa Kiongozi ningemtimua

Mwakalebela X Robertinho Sss Makamu Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Yanga, Fredrick Mwakalebela

Wed, 11 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kama angekuwa kiongozi wa Simba SC basi tayari angekuwa amemtimu kocha wa Simba Robertinho kwasababu ni mchekeshaji (Comedy).

Akizungumza kupitia bongo5 Mwakalebela amekiri kuwa Simba SC ipo vizuri na ina wachezaji wazuri lakini tatizo la Wekundu hao wa Msimbazi ni benchi la ufundi (technical bench)

Mwakalebela amegusia suala la Mwamuzi akidai haelewi “kama wanakulaga (Simba) mayai na waamuzi sijui lakini kuna fairness fulani wanakosa. Marefarii sijui wana tatizo gani, nashindwa kuelewa kwanini kwenye mechi za Simba tu”

Aidha Makamu Mwenyekiti huyo wa zamani wa Yanga amesema haoni nafasi ya Simba kufika nusu fainali wala robo ya CAF Champions League kama Aish Manula hatokaa golini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live