Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwakalebela: Mzize alikuja Yanga bila viatu

Mzize Rteee.jpeg Clement Mzize

Sun, 25 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Yanga SC, Fredrick Mwakalebela amefunguka namna walivyompokea mshambuliaji kinda wa Klabu hiyo, Clement Warid Mzize ndani ya klabu hiyo akitokea Iringa.

Mwakalebela amesema hayo wakati akifanyiwa mahojiano na kimoja kimoja cha habari nchini kuhusu mafanikio ya Yanga msimu uliopita na maandalizi yao kuelekea msimu ujao.

”Clement Mzize, mimi na Dkt. Mshindo Msola tunatoka Iringa, tumeambiwa tunawaleteeni Mzize tumeshamlipia na nauli nyie mpokeeni, tukampkea mimi na Dkt Msola.

Mwakalebela ameongeza ”Kuna siku tumekwenda mazoezini akasema mimi nataka kurudi Iringa, mimi bwana sina hata Viatu, Dkt Msola akapiga simu kwa ‘financial director’ akasema jamani naomba huyu jamaa kila wiki muwe mnampa laki mbili (tsh 200,000).

”Baadaye tukamuuliza Kocha Mwinyi Zahera unamuonaje Mzize akasema ni mchezaji mzuri.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: