Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwadui yaiduwaza Dodoma Jiji

735aece9418f7e533a05c7cc4922299d.png Mwadui yaiduwaza Dodoma Jiji

Fri, 8 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

BAO pekee lilofungwa na Wallace Kiango limeiwezesha Mwadui kuibuka na ointi zote tatu baada ya kuifunga Dodoma Jiji katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Mwadui Compex mkoani Shinyanga jana.

Kiango alipachika bao hilo dakika ya 87 akitumia vema makosa ya kushindwa kujipanga yaliyofanywa na safu ya ulinzi ya Dodoma Jiji katika mchezo huo uliokuwa na ushindani.

Matokeo hayo yanawafanya Mwadui kufikisha pointi 15 baada ya kucheza michezo 18, na wamepanda hadi nafasi ya 16 kwenye msimamo huku wapinzani wao Dodoma Jiji wakikalia nafasi ya tisa na pointi 22 baada ya kucheza michezo 17.

Huo ni ushindi wanne kwa Mwadui tangu ligi ilipoanza msimu mpya Septemba 6 mwaka jana, na mara ya mwisho kupata matokeo kama hayo walipocheza dhidi ya Mbeya City kwa mabao 2-1.

Michezo mingine miwili waliyoshinda Mwadui ni dhidi ya mabao 2-0 na Ihefu FC, kabla ya kuwatungua Namungo bao 1-0.

Chanzo: habarileo.co.tz