Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwadui FC kazi inayo kwa Simba

3643a1712287feb6892bbb77e2fed000.jpeg Mwadui FC kazi inayo kwa Simba

Sun, 18 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba leo inatarajia kucheza na Mwadui ya Shinyanga kwenye Uwanja wa CCM Kambarage.

Simba inaingia katika mchezo huo baada ya mchezo uliopita kuifunga Mtibwa Sugar mabao 5-0 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Simba imerejea kwa kasi kwenye mechi za Ligi Kuu ikipania kutetea ubingwa wake baada ya kumaliza mechi za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikisubiri kupangwa kwa ratiba ya robo fainali.

Kocha wao Didier Gomes amejinasibu kuwa wanahitaji kutetea ubingwa wao wa ligi, ambao wameuchukua kwa misimu mitatu mfululizo, hivyo kila mechi inayokuja mbele yao wamejizatiti kushinda ili kurejea kileleni, nafasi ambayo inashikiliwa na Yanga kwa sasa.

Gomes alisema hakuna mechi nyepesi na hakuna timu rahisi zaidi, isipokuwa kila dakika 90 zilizo mbele yao zinahitaji mapambano na wanachohitaji ni ushindi, ili kufikia mafanikio yao ndiyo maana wamekuwa wakipambana bila kuchoka.

“Bado ligi haijaisha, ndiyo maana tunahitaji kuongeza nguvu na kuwa na uhakika wa matokeo mazuri kila mechi. Sisi ni mabingwa watetezi kwa hiyo utaona tunahitaji kuonesha sisi ndiyo mabingwa na tunauhitaji tena ubingwa.

“Ingawa siyo rahisi ndiyo maana tumekuwa makini kabla na baada ya mechi ili kuona nini tunapaswa kufanya ili tufikie matarajio na nia tuliyonayo ndani na nje ya nchi,” alisema Gomes.

Simba inakwenda kucheza na Mwadui ikiwa katika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 49 baada ya kucheza mechi 21, Azam ya pili ikiwa na pointi 50 baada ya michezo yake 26, Yanga ipo kileleni kwa pointi 51 baada ya kucheza mechi zake 24 kabla ya mchezo wake wa jana dhidi ya Biashara.

Mwadui inayofundishwa na Amri Said inaburuza mkia katika nafasi ya 18 ikiwa na pointi 16 pekee mpaka sasa katika michezo michezo 25.

Mchezo mwingine Dodoma Jiji ikiwa nyumbani, itaikaribisha Namungo FC katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Chanzo: www.habarileo.co.tz