Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvungi kuanza majaribio ya soka la kulipwa

Cambiasso 0 Omary Mvungi (Kushoto)

Wed, 29 Dec 2021 Chanzo: eatv.tv

Mchezaji wa mpira wa miguu kutoka katika kituo cha kufunzia soka cha Cambiasso Sports, Omary Mvungi amefanikiwa kufika nchini Uingereza kwaajili ya kuanza mafunzo na majaribio ya kucheza soko la kulipwa Barani Ulaya.

Taarifa iliyotolewa na Cambiasso kupitia Ukurasa wake rasmi wa Instagrama imeeleza;

“Cambiasso Sports Management tukishirikiana na Rainbow Sports tumefanikiwa kumpeleka striker wetu kinda wa Cambiasso Sports Academy na timu ya Taifa chini ya umri wa miaka 20 nchini Uingereza kwa mwaliko wa aliyekuwa Mchezaji Nguli na Nahodha wa Chelsea na Timu ya Taifa ya Uingereza Denis Wise kwa ajili ya kupata mafunzo na misingi bora kwa ajili ya maandalizi ya kucheza soka la kulipwa (Professional Football) barani Ulaya.

Mafunzo ni muda wa miezi sita  yatayofanyika katika kituo cha Garuda programu katika kambi nahodha wa zamani wa Chelsea, Dennis Wise.

katika safari hiyo Mvungi ameambatana na Frederic Moudourou kutoka kituo cha  Rainbown cha nchini Marekani ambao wameshirikiana na Cambiasso kumtafutia fursa hiyo na kuwaahidi watanzania kuwa hatawaangusha.

Kabla ya kwenda huko, Mvungi kwa nyakati tofauti amekuwa akizitumikia timu za taifa za vijana chini ya miaka 17 na 20.

Chanzo: eatv.tv