Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvua yatibua shughuli Ruangwa

Mvua Ppic Mvua yatibua shughuli Ruangwa

Wed, 7 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Mvua kubwa iliyoshuka ghafla wilayani hapa imesimamisha shughuli zote zilizokuwa zinaendelea yakihesabiwa masaa kadhaa kufikia mechi ya Namungo dhidi ya Yanga.

Mvua hiyo imeanza kunyesha saa 8:20 mchana ilifanya watu wote ambao walikuwa wanaendelea na shughuli zao kuzisimamisha kwa muda.

Mashabiki ambao walikuwa wanapata vinywaji na chakula cha mchana eneo la stendi kuu kabla ya kwenda uwanjani nao walijikuta kwenye wakati mgumu kutokana na mvua hiyo.

Mvua hiyo ilikuwa ni ya upepo na iliwafanya watu wote wasimame na kutafuta sehemu ya kujikinga.

Mashabiki hao walisikika wakisema mvua ikatike mapema ili waende kuangalia mpira vizuri baadae.

"Mvua nayo imetoka wapi hii jamani wakati hua lilikuwa kali, tunataka tukawaone wakina Lusajo na Mayele sisi," walisikika mashabiki hao.

Namungo na Yanga zinakutana leo saa 1:00 usiku katika uwanja wa Majaliwa.

Chanzo: Mwanaspoti