Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvua yatibua mipango Yanga, Kagera Suga CCM Kirumba

Operanews1668341578901 Mvua yatibua mipango Yanga, Kagera Suga CCM Kirumba

Sun, 13 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mvua kubwa iliyonyesha leo jijini Mwanza tangu asubuhi mpaka muda huu imepunguza kasi ya watu kuja uwanjani kushuhudia mchezo wa Ligi Kuu kati ya Kagera Sugar na Yanga.

Mchezo huo utachezwa muda mfupi ujao kuanzia saa 10:00 jioni katika Uwanja wa CCM Kirumba.

Tofauti na ilivyozoeleka katika uwanja huo Yanga na Simba zinapocheza muda kama huu kunakuwa kumeshachangamka nje na ndani ya uwanja lakini hali ni tofauti siku ya leo kutokana na mvua huyo.

Mpaka sasa mvua hiyo inaendelea kunyesha huku kukishuhudiwa makundi machache ya watu nje ya uwanja wengine wakikata tiketi katika vibanda vilivyo nje ya uwanja huo.

Wafanyabiashara wakiuza miamvuli kwa mashabiki nje ya Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Miamvuli yapata soko

Kutokana na mvua inayoendelea kunyesha jijini hapa wafanyabiashara wa miamvuli wamechangamkia fursa hiyo wakiwa wamejitokeza kwa wingi nje ya Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kuwauzia mashabiki wanaofika kukata tiketi ili kuutazama mchezo wa Kagera Sugar na Yanga.

Mmoja wa wafanyabiashara wa miamvuli aliyefika, Michael Chacha amesema uwepo wa mvua umewasaidia kupata biashara ambapo wanauza bidhaa hiyo kati ya Sh 7,000 hadi 10,000.

"Tangu asubuhi nimeshauza miamvuli mingi kwahiyo hii ni fursa kwetu walau tunapata riziki kutokana na hali ya hewa ya leo," amesema Chacha.

Mfanyabiaahara mwingine, Kaonekana John amesema mara nyingi Yanga inapocheza jijini Mwanza kumekuwa na mvua jambo ambalo linaleta neema kwa wafanyabiashara na mashabiki wake kujipatia kipato.

Amesema kutokana na hali hiyo ameshukuru viongozi walioleta mchezo huo jijini hapa huku akitamba kuwa ameuza miamvuli zaidi ya 50.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live