Muuguzi Lucy Betty wa Uingereza ambaye hivi karibuni alikutwa na hatia ya kuua watoto njiti 7 na kujaribu kuua wengine 6 amehukumiwa kifungo cha maisha leo.
Kwa mujibu wa Jaji aliyetoa hukumu hiyo katika mahakama jijini Manchester, muuguzi huyo hataachiwa huru kutoka gerezani kwani aina ya hukumu aliyopewa ni ya kipekee.
Akitoa hukumu hiyo jaji Justice Goss alisema ”Lucy alifanya kampeni ya kikatili na ya kijinga ya mauaji ya watoto wadogo walio hatarini, vilevile alijua kabisa kuwa matendo yake yatasababisha mateso makubwa kimwili kwa na mateso ya kiakili.”
Muuguzi huyo anakuwa mwanamke wa tatu aliye hai kuwahi kupewa hukumu kama hii nchini Uingereza.