Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muuaji wa Simba aendelea kutupia maafande wakitoka sare na JKT Tz

Mbangula Vs JKT Tz Muuaji wa Simba aendelea kutupia maafande wakitoka sare na JKT Tz

Thu, 14 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya JKT Tanzania imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Jana Jumatano Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni Jijini Dar es Salaam.

Daniel Lyanga alianza kuifungia JKT Tanzania dakika ya 40, kabla ya mshambuliaji mwenzake, Koplo Samson Baraka Mbangula kuisawazishia Tanzania Prisons dakika ya 46.

Kwa matokeo hayo, JKT Tanzania inafikisha pointi 20 katika mchezo wa 20, ingawa inabaki nafasi ya 15 katika Ligi ya timu 16, wakati Tanzania Prisons inafikisha pointi 28 katika mchezo wa 21 na kusogea nafasi ya tano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live