Nyota wa zamani wa Arsenal, Shkodran Mustafi (30) amevamiwa na watu watatu wakati akiwa amelala nyumbani kwake karibu na jiji la Valencia nchini Hispania.
Mlinzi huyo ambaye alijiunga na klabu ya Levante mwanzoni mwa msimu ameibiwa vitu vyenye thamani ya takribani euro milioni moja.
Baadhi ya vitu vilivyoibiwa ni pesa, madini,saa na pochi. Wavamizi hao waliondoka bila kumdhuru mtu.
Mustafi amekuwa akiposti picha nyingi kwenye mtandao wa Instagram zinazoonyesha sehemu tofauti za nyumba yake na ripoti kutoka katika gazeti maarufu la michezo nchini Hispania Superdeporte inasema kuwa picha hizo huenda ziliwasaidia wavamizi hao kupata vidokezo vya namna ya kupangilia wizi huo.
Polisi wanaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.