Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mustafa atuma salamu Yanga

Beki Yanga Yassin Mustafa

Tue, 16 Nov 2021 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kukaa nje kwa muda mrefu beki wa Yanga, Yassin Mustafa na kupata nafasi ya kucheza kwenye michezo miwili ya kirafiki amesema anahitaji muda zaidi ili kurudi kwenye kikosi cha kwanza.

Yanga iliyokuwa kambini Zanzibar na kurejea juzi kisha nyota wake kupewa mapumziko ya siku mbili yanayomalizika leo, ilicheza mechi mbili za kirafiki na Mlandege na KMKM na zote kushinda, huku beki huyo akipata nafasi ya kucheza akiingia kipindi cha pili.

Katika mechi hizo zilizopigwa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar Yanga iliilamba Mlandege kwa bao 1-0 lililowekwa kimiani na Heritier Makambo kisha kuinyoosha KMKM kwa mabao 2-1 yaliyotupiwa kambani na Jesus Moloko na Fiston Mayele, huku Mustafa akiupiga mwingi.

Akizungumza na Mwanaspoti, beki huyo alisema anahitaji dakika nyongi zaidi ili aendelee kurudi kwenye ubora anahitaji kuendelea kuaminiwa hata kwenye michezo ya ligi kwa kupewa dakika chache za kucheza.

“Nimetoka nje ya uwanja kwa muda siwezi kurudi moja kwa moja nashukuru kocha kaniamini na kanipa dakika chache za kucheza nahitaji dakika zaidi hadi kwenye ligi ata dakika 10 zitanifaa kikubwa ni imani naweza kuwa bora,” amesema na kuongeza;

“Kucheza mechi za mashindano timu ikiwa inaongoza kutanipa changamoto ya kupambana kuhakikisha sifanyi makosa kwenye dakika chache nilizopewa na kunipa imani ya kuendelea kupambana ili niweze kurudi kwenye mechi za ushindani.”

Mustafa amesema ni ngumu kwake kurudi na kuaminiwa kupewa nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza moja kwa moja kutokana na ubora wa mchezaji anayecheza nafasi hiyo sambamba na ingizo jipya.

“Kuna Kibwana Shomari, David Bryson wote wako vizuri na wameweza kufanya vizuri kila walipopewa nafasi ya kuchgeza hivyo ni ngumu mimi kuingia moja kwa moja baada ya kukaa nje muda mrefu,” amesema beki huyo aliyesajiliwa Yanga msimu uliopita akitokea Polisi Tanzania.

Chanzo: Mwanaspoti