Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mussa Mgosi: Tunatakiwa kusahau yaliyopita

Simba Queensss.png Mussa Mgosi: Tunatakiwa kusahau yaliyopita

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Msaidizi wa Simba Queens, Musa Hassan Mgosi amesema kuwa wanasahau ushindi walioupata dhidi ya Yanga Princess na sasa nguvu na akili wanazihamishia kwenye mchezo wa Fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya JKT Queens utakaopigwa kesho Jumanne (Desemba 12), katika Uwanja wa Azam Complex.

Amesema hayo katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika leo Jumatatu (Desemba 11), alipokuw akieleza maandalizi ya kikosi chake kuelekea mchezo wa kesho, baada ya Simba Queens kuibanjua Yanga Princess kwa Penati 5-4 juzi Jumamosi (Desemba 09).

“Tukuwa mechi nzuri yenye ushindani Yanga Princess ambayo naitambua mimi, wamejitahidi kuleta changamoto lakini sisi tumeonyesha mabadiliko makubwa tulijandaa kupata ushindi ili kuendelea kwenye hatua inayofuata.

“Tunakwenda katika mchezo wa Fainali, inabidi kusahau yote yaliyotokea katika mchezo wa juzi Jumamosi, hapa tunakwenda katika mchezo muhimu zaidi ambao tunatakiwa kupambana na kupata ushindi ili kutwaa ubingwa wa Ngao ya Jamii msimu huu” amesema Mgosi

Naye Kocha Mkuu wa JKT Queens, Ester Chabruma, amesema anawapongeza waliondaa Ngao ya Jamii kwa kutambua umuhimu wa michuano hii kwa wanawake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live