Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Musonda kuleta straika Yanga

IMG 5437 Musonda Goal.jpeg Musonda kuleta straika Yanga

Wed, 11 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Yanga Miguel Gamondi alishakiri kwamba washambuliaji wake bado hawajamkuna kwa kumpa ule ubora ambao anautaka kulingana na michuano mbalimbali anayoshiriki.

Alipoondoka Fiston Mayele,mashabiki wa Yanga waliamini kuwa Kennedy Musonda ndio atavaa viatu vya Mayele ila hali imekuwa tofuati na kiwango cha Musonda kimekuwa ni maji kupwa na maji kujaa.

Kwa aina hii ya kiwango cha Musonda ni wazi kuwa yeye mwenyewe ataleta upenyo ama urahisi wa Yanga kuleta mshambuliaji mwengine. Kwa maana nyepesi ni kwamba kiwango cha Musonda kitaleta straika mwingine.

Hadi sasa katika mechi tano za Ligi Kuu Kennedy Musonda amefunga goli moja na Assist. Mbaya zaidi kuna viungo wanaifanya kazi yake hivyo hiyo inakuwa hatari kwake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live