Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Musonda atoa ahadi nzito kwa Wananchi

Musonda Kennedy Med Kennedy Musonda

Wed, 28 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mehambuliaji wa Yanga, Kennedy Musonda ambaye ni miongoni mwa wafungaji katika ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya CR Belouizdad wikiendi iliyopita, amefunguka mambo kadhaa kuhusu maisha yake ndani ya Young Africans SC na anachokiona msimu huu katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kufuzu robo fainali.

Musonda ambaye huu ni msimu wake wa pili ndani ya kikosi cha Young Africans SC, tayari amehusika kwenye magoli 11 kwa maana ya kufunga na kutoa asisti, akicheza mechi 17.

Nyota huyo raia wa Zambia, alikuwepo msimu uliopita wakati Young Africans SC ikicheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na kushuka nafasi ya pili.

Kuelekea mchezo wa mwisho wa Kundi D ugenini dhidi ya Al Ahly utakaochezwa Ijumaa ya wiki hii nchini Misri, Musonda ametoa ahadi kwamba, Yange ikiwafunga wapinzani weo hao na kuongoza kundi, basi ataimba kwani anapenda sana muziki hasa wa Tanzania.

Hapa Musonda anaanza kwa kusema: “Tuna furaha tunakwenda kucheza robo fainali, unajua kila mchezo ni tofauti, kila mchezo ni mkubwa, lakini inakuwa ni namna gani ya kwenda kuukabili, siwezi kusema ilikuwa mechi rahisi (dhidi ya CR Belouizdad), lakini naweza kusema tulitumia nafasi na mbinu vizuri ndiyo maana ikaonekana rahisi kufunga magoli.

“Kitu cha muhimu ni kwenda kwa hatua, hata msimu uliopita tulifanikiwa kucheza fainali, msimu huu tunaweza kusema hivyo lakini lazima twende hatua kwa hatua.

“Mwanzo ilikuwa ni kufika hatua ya makundi, hivi sasa tumeingia robo fainali, kila hatua ni muhimu, hivyo kwa sasa kitu muhimu ni kwenda nusu fainali, baada ya nusu fainali, tutazungumzia fainali.

KUHUSU MECHI ZA KIMATAIFA KUPEWA MAJINA MAALUM

“Nadhani kwetu kitu cha umuhimu zaidi ni kuwa karibuni na mashabiki, inapotokea siku ya mtu, tunaichukulia mechi kwa umuhimu mkubwa sana, nadhani hii inawafanya mashabiki kuwa karibu na wachezaji, ni kitu kizuri kwetu.

ANAZUNGUMZIAJE KUHUSIKA KWENYE MAGOLI 11 KATIKA MECHI 17

“Kwangu kitu cha umuhimu ni kuisaidia timu, sikuwa nafahamu hiyo rekodi ninayoishikilia kwa sababu mimi nafanya kila liwezekanalo kuisaidia timu ishinde na sio mafanikio binafsi.

ANAYAONAJE MAZINGIRA YA TANZANIA

“Watu wa hapa ni wazuri, utamaduni mzuri, hali ya hewa siyo tofauti, kitu cha tofauti ni mashabiki kulinganisha na nilipotoka, msisimko walionao watu katika soka hapa nadhani ni kwa kiwango cha juu, hivyo unafahamu watu wanakupa msisimko unapaswa kuwarudishia unapokuwa uwanjani.

PRESHA YA MASHABIKI HAIMPI WASIWASI

“Unajua unapokuwa na majukumu mwili nao unafahamu hilo, kusipokuwa na mashabiki kunaboa, lakini mashabiki wakiwepo, kile wanachokuambia kiwe kibaya au kizuri, kinakupa nguvu ya kupambana, hivyo suala la presha halinisumbui.

AUCHO NI MTU WA AINA GANI

“Ni mtu mzuri, muwazi, anakueleza kitu kwa uwazi, kama hiki hakipo sawa anakwambia, amenyooka, siyo mtu wa kuzungumza pembeni, hata kama kitu kibaya, atakwambia ukweli.

ANAMZUNGUMZIAJE IBRAHIM BACCA AKIWA UWANJANI

“Ni mzuri, kijana mdogo mwenye kipaji, ana moyo wa kujituma, hivyo ndivyo ninavyoweza kusema kuhusu Bacca.

CHAKULA ANACHOPENDA

“Napenda chai na chapati, kule Zambia chapati hazipatikani sana, Tanzania ndiyo wanapenda sana, Zambia siyo sana.

KUHUSU MATAJI MSIMU HUU

“Kidogokidogo, tutashinda tu, sisi tunafurahia sapoti inayotoka kwa mashabiki wa Yanga, pia tunafurahi sapoti inayotoka kwa uongozi na makocha, inatupa nguvu ya kucheza mechi zetu.

ALICHOPANGA KUKIFANYA TUKIIFUNGA AL AHLY

“Napenda muziki, muziki unatupa mzuka, unatoa mawazo, mimi napenda mziki. Nawapenda wasanii wote kama Diamond, Zuchu, Harmonize, nadhani mziki wa Tanzania ni mzuri sana. Tukiwafunga Al Ahly nitaimba.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live