Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Musonda ataja sababu ya kutwaa bao bora

Kennedy Musonda Bao Bora Kennedy Musonda

Wed, 24 May 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya bao lake alilofunga dhidi ya Marumo Gallants FC kuchaguliwa kuwa bao bora la wiki ya mechi za nusu fainali mshambuliaji Kennedy Musonda amesema ni majibu ya upambanaji wake huku akiahidi kuendelea kuwa bora.

Bao hilo la pili la Yanga kwenye nusu fainali ya pili Kombe la Shirikisho Afrika lililofungwa na Musonda akipokea pasi ya Fiston Mayele katika Uwanja wa Royal Bafokeng katika mechi hiyo bao la kwanza lilifungwa na Fiston Mayele.

Akizungumza na Mwanaspoti, Musonda alisema ataendelea kupambana kila anapopata nafasi ya kucheza majibu yake yatakuwa kama ilivyotokea kwenye mchezo huo na kufanikiwa kufunga bao bora.

"Tuzo katikati ya mashindano inaongeza morali kwa mchezaji hivyo ni moja ya nguvu kazi kwangu kuendelea kupambana na kuamini kila kitu kinawezekana nawashukuru wachezaji wenzangu kwa ushirikiano wanaonionyesha naamini tutajenga kilicho bora;

"Yanazungumzwa mengi kuhusu mimi kutokucheza mara kwa mara ninachoweza kuwaaminisha ni kwamba mimi ni mchezaji wa Yanga na ninaaminiwa na kocha kwa asilimia kubwa kinachotokea ni mipango ya benchi la ufundi kuamua kumtumia nani na nani aanzie benchi."

Musonda alisema Yanga imecheza mechi nyingi mfululizo na zote zina uhitaji wa matokeo mazuri ili waweze kuendelea kusonga mbele hivyo benchi la ufundi limekuwa likitumia wachezaji kwa kuzingatia nguvu kazi.

"Yanga sasa tuna fainali mbili zote zinaitaji matokeo mazuri ambayo ni kutwaa mataji kocha amekiwa akizungumza nasi kama wachezaji namna ya kutunza nguvu ili kuweza kufikia malengo hivyo naamini kila nafasi ntakayokuwa naipata ya kucheza nitajiweka kwenye ubora na kuwapa majibu kwa mafanikio hao wanaamini nipo benchi kiwango kimeshuka." alisema Musonda.

Tuzo ya Musonda kwa Yanga inakuwa ni ya pili katika hatua hiyo baada ya mechi ya kwanza kwa Mkapa Azizi KI alibeba tuzo hiyo waliposhinda mabao 2-0 huku la pili likiwekwa na Bernard Morrison.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: