Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Musonda anataka bao la mapema

Musonda 68 Musonda anataka bao la mapema

Wed, 17 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kutwaa taji lake la kwanza akiwa na Yanga mshambuliaji Kennedy Musonda amefunguka kuwa ametua timu bora yenye uchu wa mataji anajiona akitwaa taji la Afrika na kuandika rekodi mpya.

Kuhusu mechi ya Marumo Jumatano hii, Musonda alisema wakifunga bao moja la dakika za mapema watakuwa na wakati mzuri wa kuzuia mashambulizi ya wapinzani lakini kama watacheza bila ya kufunga watakuwa na presha kubwa.

"Tumetwaa taji tukiwa na michezo miwili mkononi na tunaenda kucheza mchezo wa marudiano Jumatano dhidi ya Marumo tukiwa kwenye hali nzuri ya ushindani na malengo yetu ni kutinga hatua inayofuata;

"Haitakuwa rahisi tunatarajia ushindani mkubwa kutoka kwa wapinzani wetu kama walivyotushangaza nyumbani hatukutarajia kukutana na ushindani kama waliotupa hivyo tumejiandaa vyema kwa kutambua tunakutana na timu ya aina gani." alisema.

Musonda alisema malengo yao wachezaji na benchi la ufundi ni kuona wanapata matokeo mazuri na kutinga hatua inayofuata kwa heshima huku akisisitiza kuwa kwa walipofikia kila mchezo wanaocheza wanauchukulia kama fainali.

"Yanga ni timu ambayo kutokana na matokeo mazuri tunayoyapata tunakutana na changamoto ya kukamiwa na wapinzani mchezo uliotupa ubingwa hakuna aliyetarajia kama angeona ushindani mkubwa kama ule;

"Hivyo hata Jumatano kutakuwa na mchezo mzuri sana utakuwa ni wa ushindani kwa pande zote mbili hatutatumia vibaya nafasi tutakazotengeneza tunahitaji bao moja la mapema ili kujiweka katika nafasi nzuri" alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: