Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Musonda akichafua Zambia, Chama akalia mbao ndefu

Musonda Chama Musonda akichafua Zambia, Chama akalia mbao ndefu

Wed, 10 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Taifa ya Zambia 'Chipolopolo' imecheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Cameroon huko Jeddah Zambia na kutoa sare ya kufungana bao 1-1 ikiwa ni maandalizi ya kuelekea kwenye michuano ya Fainali za AFCON 2023 zinazotarajiwa kuanza kutimua vumbi Jumamosi, Januari 13, 2023.

Patson Daka ndiye alianza kufunga bao la kuongoza kwa Zambia dakika ya 11 tu ya mchezo kabla ya mlinzi wa Cameroo, Darlin Yongwa kuifungia Cameroon bao la kusawadhisha dakika ya 20 .

Mshambuliaji nyota wa Klabu ya Yanga, Kennedy Musonda aliingia dimbani dakika ya 59 kuchukua nafasi ya Patson Daka.

Nyota wa zamani wa Simba SC, Larry Bwalya amecheza dakika tisini katika mchezo huu wa kirafiki. Kipenzi cha mashabiki wa Simba, Clatous Chama hakupata nafasi ya kuingia Dimbani katika mchezo huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live