Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Musonda afunguka kuhusu Gamondi kumpiga benchi

MUSONDA ER.jpeg Musonda afunguka kuhusu Gamondi kumpiga benchi

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Kennedy Musonda amefunguka kuhusu kupigwa benchi na kocha wake, Miguel Gamondi na badala yake kocha huyo raia wa Argentina kupendelea kuanza na kinda Mtanzania, Clement Mzize.

Akizungumzia hilo, Musonda ambaye ni raia wa Zambia amesema kuwa Yanga ina wachezaji wengi wazuri na kila mmoja anaonyesha uwezo wake hivyo ni jukumu la kocha kuamua ni mchezaji yupi aanze naye kutokana na mpango kazi wake kuelekea kwenye mchezo husika.

"Klabu ina wachezaji wengi ambao wanacheza wakati mwingine mwalimu anafanya rotation ya wachezaji ili wengine pia wapate nafasi ya kucheza ila lengo la wachezaji wote ni kuipambania timu.

"Yanga ni timu kubwa na ina malengo makubwa hivyo ukiwa mchezaji wa Yanga sc tayari unakuwa ushajiandaa kuhakikisha unasimamia sera ya timu.

"Presha ya mashabiki pia ipo kwasababu wanataka matokeo mazuri na siku zote tunajitahidi kupambana ili kuwapa matokeo chanya," amesema Kennedy Musonda.

Tangu kuondoka kwa aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele, Yanga ilimsajili Hafiz Konkoni kwa ajili ya kusaidizana na Musonda lakini wawili hao wote inaonekana mwalimu Gamondi bado hajawaamini vya kutosha hivyo kuamua kumtumia Mzize kama chaguo lake namba moja.

Zipo taarifa kuwa, Gamondi ameueleza uongozi wa yanga kuwa anaomba aongezewe washambuliaji wengine kwenye dirisha dogo la Ligi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: