Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Musonda: Hatuna pesha, tumeanza vibaya, tutamaliza vizuri

Dg Musondaa Musonda: Hatuna pesha, tumeanza vibaya, tutamaliza vizuri

Thu, 7 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa kati wa kikosi cha Yanga, Kennedy Musonda amesema kuwa hawana presha na mchezo wao wa kesho dhidi ya Medeama FC ya nchini Ghana kwani wao kama wachezaji wamejiandaa vyema kwa ajili ya kupambana na kupata ushindi.

Musonda amesema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari nchini Ghana kuelekea mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi huku akiongeza kuwa, licha ya kuanza vibaya katika michezo yao miwili ya awali, wana uhakika watavuka hatua inayofuata.

“Kama wachezaji tumeweka umakini kwenye mchezo wa kesho na kuhakikisha tunapata matokeo mazuri hapa. Tunafahamu mashabiki wanategemea mazuri mengi kutoka kwetu na sisi tunategemea mengi kutoka kwetu kama wachezaji.

“Tunajua ni mchezo mkubwa na mgumu kwetu lakini hatuna presha. Hili ni soka kuna wakati unaweza usianze kama unavyotarajia lakini jambo muhimu ni jinsi gani unavyomaliza mashindano na sisi tumedhamiria kumaliza vizuri,” amesema Musonda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live