Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Musiala atabiri bingwa UEFA

Jamal Musiala Nyota wa Bayern Munich, Jamal Musiala

Tue, 26 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Nyota wa Bayern Munich, Jamal Musiala amechagua timu tatu ambazo anadhani zinaweza kushinda Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani, aliyekulia jijini London, ana matumaini ya kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu inayotarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Wembley.

Wakati Musiala akiwa na ndoto za kushinda Ligi ya Mabingwa ambayo anaona kama taji muhimu zaidi katika historia ya soka lake, ameichagua Real Madrid, Manchester City na Arsenal kuwa zina nafasi kubwa ya kubeba taji hilo msimu huu.

Akizungumza na mtandao wa Abendzeitung, kijana huyo alisema: “Ligi ya Mabingwa ni taji muhimu zaidi katika soka kwa ngazi ya klabu. Nina malengo ya kubeba taji hili, fainali ya mwaka huu itakuwa Wembley, huu ni uwanja maalumu kwangu, tutapambana kwa kila kitu, tutajitolea kwa ajili ya timu, muhimu wachezaji kuwa fiti zaidi.”

Mbali na kujipigia debe, kinda huyo alitoa nafasi tatu kwa timu pinzani ambazo zinaweza kufanya vizuri kwenye mashandano hayo mwakani.

“Nadhani Real Madrid na Man City ndizo zinaweza kufanya vizuri. Lakini hata Arsenal pia inacheza soka zuri chini ya Mikel Arteta.”

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 ana kiwango kizuri msimu huu, kwani amefunga mabao matano na kutoa asisti tatu katika mechi 18 mashindano yote aliyocheza.

Ndiye mfungaji bora wa tatu wa Bayern aliyefunga Bundesliga baada ya Harry Kane na Leroy Sane.

Chanzo: Mwanaspoti