Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Murray kumnyoosha Djokovic? Raducanu atupwa nje!

Murray Andy Murray Andy Murray

Wed, 4 May 2022 Chanzo: eatv.tv

Nyota wa Tennis raia wa uingereza Andy Murray sasa atakutanana mpinzani wake wa siku nyingi Novak Djokovic alhamis wiki hii kwa mara ya kwanza tangu walipokutana mwaka 2017.

Murry amemshinda Denis Shapovalov wa Canada kwenye michuano ya madrid open inayoendelea nchini Hispania. Murray mwenye miaka 34, alionyesha kiwango cha juu na kushinda kwa seti mbili kwa moja kwa kupata alama 6 -1, 3- 6 na 6 - 2 dhidi ya mchezaji huyo nambari 16 duniani kwa ubora Denis Shapovalov.

Kwa upande wa Mserbia Novak Djokovic yeye alianza safari yake kwa ushindi wa seti mbili mfululizo kwa kupata alama 6-3 na 6-2 dhidi ya mfaransa Gael Monfils. Sasa bingwa huyo mara 20 wa Grand slam atacheza na Murray ambaye amemfahamu tangu wakiwa watoto na wamekutana mara 36 katika maisha yao ya kucheza tennis.

Kwa upande wa wanawake Mchezaji namba moja wa Uingereza Emma Raducanu ameshindwa kufuzu hatua ya robo fainali ya Madrid Open baada ya kutolewa na Anhelina Kalinina wa Ukraine.

Raducanu mwenye umri wa miaka 19 anayeshika nafasi ya 11 kwa ubora duniani kwa wanawake, alipoteza mchezo huo kwa seti mbili kwa moja baada kufungwa kwa alama 6-2, 2-6 na 6-4 na kisha kutupwa nje ya michuano hiyo.

Chanzo: eatv.tv