Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muonekano mpya wa Uwanja wa Barcelona 'Spotify Camp Nou'

Future Camp Nou Spotify Camp Nou.

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Barcelona imeingia mkataba na kampuni ya Limak construction kwa ajili ya ukarabati na upanuzi wa uwanja wa Spotify Camp Nou unaotarajiwa kukamilika mwaka 2026.

Idadi ya watazamaji itaongezeka kutoka 99,000 hadi 105,000 huku paa jipya litajengwa kufunika sehemu ya juu ya uwanja likiwa na mita za mraba 45,000.

Klabu hiyo inatarajia kuandaa mechi za Kombe la Dunia la 2030 na pengine hata fainali za kombe hilo huku uwanja huo mpya unatarajiwa kuwa na mfumo wa umwagiliaji unaotumia maji ya chini ya ardhi na paneli za jua ambazo zitatoa nishati inayohitajika uwanjani hapo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live