Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muller ndo basi tena Bayern

Thomas Muller Bayern Munich 3327746 Thomas Muller

Tue, 5 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Harry Kane anaweza kumpoteza Thomas Muller kwani anatakiwa kuondoka Bayern Munich huku akihusishwa na Manchester United.

Mshindi huyo wa Kombe la Dunia mwaka 2014 amekosa nafasi ya kudumu tangu Kane alipowasili katika dirisha la usajili lililopita.

Mkongwe huyo pia amekosa nafasi kutokana na uwepo wa kinda wa miamba hiyo Jamal Musiala, na winga wa zamani wa Manchester City, Leroy Sane, wengine ni Kingsley Coman, Serge Gnabry, na Eric Maxim Choupo-Moting.

Mkongwe wa soka Ujerumani Lothar Matthaus, amependekeza Muller afikirie kuondoka Bayern akasake changamoto sehemu nyingine baada ya kupata mafanikio na miamba hiyo.

Gwiji huyo aliyewahi kubeba Kombe la Dunia akiwa na kikosi cha Ujerumani, amemshauri Muller kuitolea macho Ligi ya Marekani (MLS) akaungane na nyota wa Inter Miami, Lionel Messi.

Matthaus alisema kupitia Sky Sport ya Ujerumani: “Akiwa Bayern Munich, hatapata tena dakika kama ilivyokuwa miaka miwili iliyopita. Kama anataka kucheza kama alivyofanya miaka miwili iliyopita, basi anatakiwa kuondoka. Huo ndo ukweli, Muller anapitia wakati mgumu uamuzi unahitajika.”

Kwa mujibu wa Bild, kocha Erik Ten Hag anavutiwa na Muller na anatamani ajiunge matajiri wa Jiji la Manchester mwaka 2024.

Mdachi huyo alitamani kumsajili katika usajili uliopita hata hivyo uhamisho wake ukashindikana kwani Bayern ilikuwa haina nia ya kumuuza kipindi hiki.

Hata hivyo, Man United inaweza kujaribu kumsajili ili kutatua safu ya ushambuliaji kwani Marcus Rashoford, kiwango bado hakiridhishi huku Rasmus Hojlund bado akiendelea kusuasua kwenye ligi tangu alipotua.

Muller amekuwa sehemu ya mafanikio ya muda mrefu ya Bayern na ameisadia kubeba mataji mengi kama Bundelsiga na Ligi Mabingwa Ulaya.

Chanzo: Mwanaspoti