Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muller afikisha mechi 600 Bayern

MULLER Kiungo ,shambuliaji wa Ujerumani na Bayern Munich, Thomas Muller

Mon, 22 Nov 2021 Chanzo: ippmedia.com

Thomas Muller amekuwa mchezaji wa kwanza kufikisha michezo 600 kwa bayern Munich tangu kuundwa upya kwa Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundasliga) mwaka 1963 baada ya kucheza dhidi ya Augusburg siku ya Ijumaa.

Muller alikulia katika akademi ya Bayern na alichezeshwa mchezo wake wa kwanza wa Bundesliga na Jurgen Klinsmann Agosti mwaka 2008, lakini alicheza mechi nne tu kati ya 34 msimu huo.

Kuwasili kwa Louis van Gaal kulimpa nafasi Muller msimu wa 2009-10 akipata nafasi ya kucheza mara kwa mara kwenye kikosi hicho.

Msimu huu tayari amehusika katika mabao 17 kwenye Bundesliga akipitwa na Mohamed Salah pekee kwa bara la Ulaya aliyehusika kwenye mabao 20.

Katika umri wake wa miaka 32, Muller sasa anaiwania rekodi ya kuwa mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi kwa Bayern, ambayo iliwekwa na golikipa, Sepp Maier aliyecheza mechi 700.

Chanzo: ippmedia.com