Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mukwale aanza moto wake huko Misri, atupia Simba ikishinda 2-1

Mukwale Aanza Moto Wake Huko Misri, Atupia Simba Ikishinda 2 1.png Mukwale aanza moto wake huko Misri, atupia Simba ikishinda 2-1

Tue, 30 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji mpya wa Simba SC ameanza kuonesha makali yake baada ya jana Julai 29, 2024 kuchagiza ushindi wa 2-1 wakati Wekundu hao wa Msimbazi walipokuwa wakipepetana na Aladalah Club ya Sudan.

Ushindi huo ni wa tatu mfufululizo baada ya kucheza michezo miwili nchini humo na yote kupata ushindi ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya msimu ujao wa 2024-25.

Magoli hayo ya Simba yalifungwa na Steven Mukwala na Joshua Mukwale.

Awali, Simba walicheza na Canal SC na kuibuka na ushindi wa 3-0 mabao yakiwekwa kimiani na Ahoua Jean Charles aliyetupia mawili na Augustine Okejepha akishindilia msumali wa mwisho.

Mchezo uliofuata, Simba alicheza juzi Julai 28 na Telecom Egypt na kuibuka na ushindi wa 2-1 mabao yakifungwa na Valentino Mashakana na Ladaki Chasambi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live