Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mukwala aitaka namba ya Onana

Mukwala Onana Mukwala aitaka namba ya Onana

Fri, 12 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Winga mpya wa Simba, Joshua Mutale imeelezwa amechagua kuvaa jezi namba saba, iliyokuwa inavaliwa na kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Willy Essomba Onana ambaye anatajwa kutokuwa kwenye mipango wa kikosi hicho kwa msimu ujao, huku Steven Mukwala akiubeba mzigo wa Clatous Chama aliyehamia Yanga.

Simba inadaiwa inapambana kumtoa kwa mkopo Onana, ingawa haijajulikana ni timu ipi, japo inatajwa timu za nje zaidi kwani ndio msimamo wa nyota huyo kutoka Cameroon aliyejiunga na Simba msimu uliopita akitokea Rayon Sports ya Rwanda akiwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu nchini humo.

Mutale alikuwa anaivaa jezi namba saba katika timu aliyotoka ya Power Dynamos ya Zambia, hivyo baada ya kuona aliyekuwa anaivaa hataendelea kusalia klabuni hapo akaomba akabidhiwe yeye.

Mmoja wa kiongozi wa timu hiyo alisema; "Imekuwa rahisi kwa Mutale kukabidhiwa jezi namba saba, kwa sababu Onana hatakuwepo, vinginevyo ingekuwa ngumu," alisema kiongozi huyo na kuongeza;

"Kwa upande wa Steven Mukwala ameomba apewe jezi namba 17 iliyokuwa ikivaliwa na Clatous Chama, pia kwa sababu ilikuwa wazi akapewa."

Mwanaspoti linafahamu kuwa, Chama mara baada ya kutua Jangwani ameomba kuendelea kuvaa jezi namba 17 aliyokuwa akiitumia Simba, ambayo awali ilikuwa ikitumiwa na Farid Mussa ndani ya kikosi cha Yanga na kiungo mshambuliaji huyo wa zamani wa Azam, atatafutiwa namba nyingine ilimradi mambo yaendelee.

Hata hivyo, katika mazoezi ya juzi kambini Avic, Kigamboni, Chama alionekana kutinga na jezi namba 20 iliyokuwa ikitumiwa na Zawadi Mauya, huku Prince Dube akiwa na namba 29 aliyokuwa akiitumia tangu akiwa Azam, wakati Andambwile akiwa na namba 2.

Chanzo: Mwanaspoti