Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mukombozi mzuka umepanda Namungo

Mukombozi Pic Derrick Mukombozi.

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa Namungo Mrundi, Derrick Mukombozi amesema sababu ya kuonekana zaidi akishambulia licha ya kucheza kama beki wa kati ni kutokana na uchu alionao wa kuipatia timu hiyo matokeo mazuri hususan anapoona mambo yamekuwa ni magumu kwao.

Mukombozi aliyejiunga na timu hiyo msimu huu akitokea Nkana ya Zambia amefunga mabao mawili ya Ligi Kuu Bara huku akiwa ni mchezaji tegemeo wa kikosi cha kwanza chini ya aliyekuwa Kocha Mkuu, Cedric Kaze na hata alipoachiwa Denis Kitambi.

“Unajua unapokuwa beki unaona kila kitu kinachoendelea mbele sasa kuna muda ninaona kabisa nikienda ninaweza kufunga na nashukuru kweli nikifanya hivyo nasababisha madhara kwa wapinzani wetu jambo ambalo kwangu binafsi najivunia,” alisema.

Beki huyo wa kati alieleza malengo yao ni kuona kikosi hicho kinaendelea kuonyesha ushindani katika kila mchezo hivyo bado wana kazi kubwa ya kufanya kwa sababu upinzani umekuwa ni mkubwa bila ya kujali unacheza nyumbani kwako au ugenini.

“Tangu nimejiunga hapa Tanzania nimejionea mambo mengi sana ila kitu ambacho kimenivutia ni kuona mashabiki wakipenda sana mpira na kutoa hamasa kubwa kwa timu wanazozishabikia kwani hii ni tofauti kidogo na nchi nilizotokea,” alisema.

Mbali na kuichezea Nkana nyota huyo, ila aliwahi pia kuitumikia Prisons Leopards ya Zambia na LLB Academic ya kule kwao Burundi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live