Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mukoko hayumo kilele wiki ya Mwananchi

Mukoko.png?fit=735%2C424&ssl=1 Kiungo wa Yanga, Mukoko Tonombe anatarajiwa kukosekana Jumapili ya Agosti 29

Sat, 28 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo kipenzi wa Mashabiki wa Yanga, Mukoko Tonombe atakosekana kesho Jumapili katika Kilele cha Wiki ya Mwananchi.

Sababu kubwa ya Mchezaji huyo kukosekana katika tukio hilo la kihistoria kwa Yanga ni kutokana na Mchezaji huyo kuitwa katika maandalizi ya timu ya Taifa.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa nyota huyo atakosekana kwa sababu ya majukumu ya timu ya Taifa.

"Mukoko anaondoka kuelekea Congo kwenye majukumu ya timu ya Taifa hivyo ni mchezaji pekee atakayekosekana kesho," amesema.

Katika hatua nyingine Mwakalebela amewataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi ili kutoa sapoti katika kikosi hicho kinachotarajiwa kucheza na Zanaco ya Zambia.

"Nawasihi mashabiki wa Mwanza, Mbeya, Iringa, Dodoma na kwingineko kujitokeza kwa wingi ili kujionea tamasha kubwa la kihistoria, "amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live