Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mukoko amtia Kaze lawamani Yanga

Kaze Pic Mukoko Data Mukoko amtia Kaze lawamani Yanga

Fri, 19 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Olipa AssaMore by this Author Dar es Salaam. Sare ya tatu mfululizo kwa Yanga juzi imekuwa mwiba mchungu kwa kocha Cedric Kaze, huku mashabiki wakiwa na hasira juu ya upangaji wake.

Kaze, ambaye ameiongoza Yanga kucheza bila kupoteza mchezo wowote wa kimashindano, alijikuta katika wakati mgumu baada ya kikosi chake kutangulizwa kwa mabao 3-2 baada ya dakika 45 na Kagera Sugar.

Katika mchezo huo uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa. Dar es Salaam.

Mchezo huo uliomalizika kwa sare ya mabao 3-3 ulimfanya Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla kutoka chini ya ulinzi baada ya mashabiki waliokuwa na hasira kumzonga.

Lakini lawama pia zilikwenda kwa Kaze, ambaye kwa mshangao aliamua kumwacha nje kiungo mkabaji, Mukoko Tonombe na kumtumia Zawadi Mauya katika kiungo.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz