Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mukoko aletewa kocha mpya

Mukoko Pic Data Mukoko aletewa kocha mpya

Thu, 20 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

YANGA ipo jijini Dodoma tangu Jumanne asubuhi na jana ilicheza dhidi ya JKT Tanzania na kupata ushindi wa mabao 2-0 lakini viungo wao Mukoko Tonombe na winga Tuisila Kisinda wana ugeni mkubwa kichwani mwao wakiletewa Muargentina aliyewahi kufanya kazi Valencia hata mabingwa wa Italia msimu huu Inter Milan.

Mukoko ndio hasa mgeni huyo anamhusu na wakati akifurahia kuitwa kwa mara ya pili katika kikosi chao cha Taifa DR Congo, Chama cha Soka nchini humo kimempa ajira kocha mkongwe Héctor Cúper.

Cúper anatua DRC maarufu kama Leopard akichukua nafasi ya kocha mkongwe mzawa Christian Nsengi-Biembe aliyetimuliwa miezi michache kufuatia taifa hilo kushindwa kufuzu Fianali za Mataifa Afrika mwakani.

Mukoko lazima ugeni huu utamshtua kwani Cúper atakuwa jukwaani akiwaangalia wachezaji wa taifa hilo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Tunisia Juni 10, chini Tunisia. Mbali na kufanya kazi katika klabu kubwa za Ulaya hapa Afrika, Cúper mara ya mwisho kufanya kazi Misri na timu ya taifa hilo kwa miaka ya 2015-18.

Akizungumzia ujio huo Mukoko alisema amesikia taarifa hizo na kwa sasa maamuzi hayo yataongeza ugumu zaidi katika ushindani wa namba kila mmoja akitaka kumshawishi kocha mpya.

“Hii ni hatua nzuri kama nchi kupata kocha mpya lakini kwa wachezaji huo ni ugumu mwingine ni lazima uonyeshe uwezo mkubwa kumshawishi kocha mpya unajua tukakutana wachezaji wanaocheza soka Ulaya na Afrika lakini nimejiandaa vyema,” alisema Mukoko.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz