Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mukoko Tonombe 'bye bye' TP Mazembe

Mazembe Mukoko Mukoko Tonombe

Wed, 12 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya TP Mazembe ya Congo DR inafikiria kumuuza kiungo wao, Serge Mukoko Tonombe (27) msimu ujao iwapo watapokea ofa nzuri.

Taarifa za ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa, maamuzi ya miamba hao wa Soka Afrika yanakuja baada ya Mukoko kushindwa kuonyesha kiwango bora na kuwashawishi mabosi wa klabu hiyo ambayo imeshindwa kufanya vizuri katika mashindano ya CAF.

Ikumbukwe kuwa, TP Mazembe waliondolewa katika hatua ya awali ya michuano ya Kombe la Mabingwa Afrika na Vipers United ya Uganda kisha kuangukia Shirikisho ambako pia wameondolewa huku wakipokea kichapo nje ndani kutoka kwa Yanga.

Mukoko amewahi kuichezea klabu ya Yanga iliyokuwa katika hali ngumu ya kiuchumi akitokea AS Vita ya Congo na baadae alijiunga na TP Mazembe ya Congo baada ya makubaliano na Yanga kwa kubadilishana na Chico Ushindi ambaye naye hakuweza kufanya vizuri Yanga.

Tayari Mazembe wameshaanza mkakati wa kuboresha kikosi chao kwa msimu ujao huku ikielezwa kuwa nyota wao wengi watapigwa chini ili kusafisha kikosi na kuleta majembe mapya.

TP Mazembe imeshamtambulisha aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa Timu hiyo, Lamine Ndiaye kukinoa tena kikosi hicho.

Chini ya N'Diaye, Mazembe iliwahi kushika nafasi ya pili katika mashindano ya Klabu Bingwa ya Dunia. Pia ilitwaa taji moja la Ligi ya Mabingwa Afrika lakini pia mataji mawili ya Caf Super Cup.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live