Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mukoko Tonombe aibua shangwe kwa Mkapa

Mukoko Tonombe Tr.jpeg Mukoko Tonombe aibua shangwe kwa Mkapa

Sun, 19 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa TP Mazembe, Mukoko Tonombe amepokelewa kwa shangwe na mashabiki wa timu yake ya zamani huku wenzake wakikumbana na zomea zomea.

Mazembe ndio walikuwa wa kwanza kuingia uwanjani wakitangulia makipa wao wawili kisha sekunde chache baadaye wenyeji Yanga waliingia uwanjani.

Yanga wakimtanguliza Fiston Mayele walishangiliwa kwa shangwe huku mshambuliaji huyo naye akiwaamsha mashabiki wao kuwahamasisha kuchangamka.

Baada ya sekunde chache Mazembe wakaingia kundi lingine huku wakiwa wanazomewa na mashabiki wa Yanga.

Wakati zomezomea hiyo ikiendelea Mukoko aliisitisha kwa kushangiliwa na mashabiki wa Yanga. Mukoko aliwajibu kwa kuwapigia makofi akigeukia kila jukwaa huku nao wakimshangilia kwa nguvu. Mukoko kabla ya kutua Mazembe msimu mmoja uliopita alisajiliwa hapo akitokea Yanga baada ya kuuzwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live