Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mukoko Tonombe: Mzamiru na Chama walinisumbua sana

Mukoko Tonombe: Mzamiru Na Chama Walinisumbua Sana Mukoko Tonombe: Mzamiru na Chama walinisumbua sana

Tue, 11 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota aliyewahi kukipiga Yanga SC, Mukoko Tonombe, amesema moja kati ya wachezaji waliokuwa wakimpa wakati mgumu akikutana nao ni Mzamiru Yassin na Clatous Chama.

Mukoko ameyasema hayo alipokuwa akifanyiwa mahojiano na Wasafi FM leo Juni 11, 2024 kuhusu masuala mbalimbali yahusuyo soka.

"Yule mchezaji ambaye huwa pia anacheza timu ya Taifa yule Mzamilu Yasini na Chama wale ni wasumbufu kweli ukikutana nao," alisema Mukoko.

Mukoko aliondoka Yanga na kwenda kukipiga TP Mazembe na sasa amesema yupo huru kwa timu yoyote itakayomuhitaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live