Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muigizaji Nigeria: Niko tayari kumtolea figo mume wangu kuliko baba

Muigizaji Nigeria: Niko Tayari Kumtolea Figo Mume Wangu Kuliko Baba Muigizaji Nigeria: Niko tayari kumtolea figo mume wangu kuliko baba

Thu, 9 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwigizaji maarufu kutoka nchini Nigeria, Regina Daniels amezua gumzo mitandaoni baada ya kudai kuwa yuko tayari kumtolea figo mumewe Mh.Ned Nwoko ili apone na aendelee kuishi kuliko kumtolea baba yake mzazi.

Kufuatia mahojiano yake ya hivi karibuni mrembo huyo aliulizwa swali kuwa mfano baba yake na mumewe wakiwa hospitali nani atakuwa chaguo lake la kwanza kumtolea figo na kueleza kuwa,

“Kama mama, nitatoa figo yangu kwa baba wa watoto wangu siyo kwa sababu ni mume wangu lakini kwa sababu sitaki watoto wangu wakue bila baba,” Mh. Ned Nwoko na Regina Daniels walifunga ndoa Aprili mwaka 2019 na wamebahatika kupata watoto wawili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live