Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mugalu nje wiki mbili, Dilunga wiki tatu

Mugalu Out Wachezaji wa Simba watakosekana kwa wiki kadhaa kutokana na Majeraha

Wed, 16 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Simba, Chris Mugalu atakuwa nje ya Uwanja kwa wiki mbili kuuguza jeraha la mkono, wakati kiungo Hassan Dilunga atakaa nje kwa wiki tatu baada ya kupata majeraha ya mguu.

Mugalu aliumia katika mchezo dhidi ya Mbeya Kwanza wakati Dilunga aliumia mazoezini wakati timu inajiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ASEC Mimosas jumanne iliyopita.

Daktari wa Simba, Edwin Anakret amesema baada ya wiki mbili Mugalu ataanza mazoezi pamoja na wenzake wakati Dilunga atasubiri vipimo tena kabla ya kuruhusiwa Kurudi Uwanjani rasmi.

Dkt. Anakret amesema pamoja na mambo mengine nyota hao wanaendelea vizuri na wangeweza kurudi uwanjani hata kabla ya siku hizo zilizotajwa ila wataendelea kuwa chini ya uangalizi hadi watakapokuwa fiti kabisa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live