Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mugalu aandaliwa programu maalum, Mkude ajifua na wenzake

Mugalu 2?fit=1705%2C1136&ssl=1 Mugalu aandaliwa programu maalum, Mkude ajifua na wenzake

Wed, 6 Oct 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

MSHAMBULIAJI wa Simba Chris Mugalu amepata majeruhi ya misuli hali iliyomfanya kuandaliwa mazoezi mepesi.

Mugalu ameonekana akipewa huduma ya kwanza kabla ya kuanza kupewa mazoezi hayo katika Uwanja wa Boko Veterani.

Kocha wa viungo wa Simba, Adel Zrane ameonekana akimpatia mazoezi ya kunyoosha miguu mchezaji huyo, huku akijitenga na wachezaji wenzake.

Wachezaji wengine waliokuwa wanafanya mazoezi peke yao ni Pape Sakho aliyepata majeraha kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji pamoja na kiungo Hassan Dilunga.

Kikosi cha Simba kinaendelea na mazoezi kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana, mchezo utakaofanyika Oktoba 15.

Nyota wengine waliofanya mazoezi ya nguvu chini ya kocha Didier Gomes ni kipa Beno Kakolanya, Ally Salim, Jeremia Kisubi, Ahmed Feruzi, Bernard Morisson, Jonas Mkude ambaye aliaga kambi ya Taifa Stars kwasababu za kifamilia, Ibrahim Ajib Henock Inonga, Sadio Kanoute, Pascal Wawa.

Wengine ni Hassan Dilunga, Pape Sakho, Yusuf Mhilu, Chris Mugalu na Gadiel Michael wakiungana na nyota wengine kutoka kikosi B.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz