Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mugalu, Dilunga bado sana Simba

Mugalu Out Mugalu, Dilunga hawatahusika michezo ya Simba mwezi Februari

Fri, 18 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Simba inayoondoka leo itaendelea kuwakosa nyota wake wawili wa kikosi cha kwanza, Chris Mugalu na Hassan Dilunga watakaokuwa nje ya uwanja hadi Machi huku akikosa mechi kadhaa ikiwamo kimataifa.

Simba inaenda Niger kisha kuunganisha Morocco kwenye mechi mbili za Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa Kundi D siku chache tangu itoe dozi nene kwa Asec Mimosas ya Ivory Coast katika mechi ya kwanza.

Wawakilishi hao wa nchi waliinyoa Asec mabao 3-1 na usiku wa jana ilikuwa ikimalizana na Ruvu Shooting katika mechi ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) kabla ya leo mchana kusafiri kwenda Niger kuvaana na US Gendermarin.

Lakini ikiwa kwenye maandalizi ya safari hiyo imebainika nyota wake watatu hawatakuwa kwenye msafara akiwamo Kibu Denis, Mugalu na Dilunga walio majeruhi na daktari wa timu hiyo, Edwin Anakret alifafanua kila mmoja na tatizo lake.

Anakret alisema kila mmoja anasumbuliwa na majeraha yake hivyo wataukosa mchezo ujao wa Kimataifa na mingine ya ligi.

Alisema Mugalu aliumia kidole katika mchezo na Mbeya Kwanza ambao Simba ilishinda bao 1-0 na atakuwa nje ya uwanja wiki mbili akiwa chini ya uangalizi wa daktari. Kuhusu Dilunga aliumia mguu wakiwa ma-zoe-zini kujiandaa na Asec Mimosas ambaye atakuwa nje wiki tatu. “Baada ya wiki mbili Mugalu ataanza mazoezi mepesi, lakini Dilunga atasubiri vipimo tena kabla ya kuruhusiwa kurudi uwanjani rasmi,” alisema Anakret.

Akizungumzia majeraha yake, Mugalu alisema kila jambo lina sababu zake na anaamini kwa uwezo wa Mungu atapona na kurejea tena katika majukumu yake. “Niliumia kidole cha mkono lakini kwa sasa namshukuru sana Mungu naendelea vizuri,” alisema Mugalu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live