Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mudau: Naipenda Kaizer Chiefs

Mudau Mwesz Mudau: Naipenda Kaizer Chiefs

Fri, 12 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Johnson Mudau ambaye ni baba wa beki wa kulia wa Mamelodi Sundowns, Khuliso Mudau amezungumzia mustakabali wa mtoto wake ambaye anatajwa kusepa klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu.

Mudau amesema anaipenda Klabu ya Kaizer Chiefs lakini alimruhusu mwanae kwenda kujiunga na Mamelodi Sundowns kutokana na maslahi na ubora wa timu hiyo kwa sasa.

"Naipenda Kaizer Chiefs kwa moyo wangu wote, sitaiacha klabu hata iweje lakini nilimwambia mwanangu [Mudau] aende Mamelodi Sundowns walipomtaka, ni klabu nzuri, anafuraha huko, wanashinda mataji.

"Nakumbuka alipofunga goli la kusawazisha dhidi ya Kaizer kwenye MTN8, moyo uliyeyuka, sikujua kujisikia, huenda nikajiunga nao, mybe, sijui?

“Lakini nataka abaki klabuni, sitamlazimisha kuja Soweto, anaendelea vizuri huko, na huwa nasubiri michezo yetu na sundowns, iwe ni ya eastern Cape au Cape town, huwa nafuatilia. lakini ni Mungu pekee ndiye anayejua mustakabali wake," amesema Baba yake Mudau.

Hivi karibuni Kocha wa Mamelodi Sundowns, Rhulani Mokwena alithibitisha kuwa, Mudau atajiunga na Burnley FC ya Uingereza mwishoni mwa msimu huu, na tayari Mamelodi wamemsajili Zuko Mdunyelwa kuziba pengo lake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live