Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mudathri apewa u-MVP

Mudathir Yahya Simuu Kiungo wa Yanga, Mudathir Yahya

Wed, 5 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Msimu wa 2023/2024 umetamatika rasmi majuzi baada ya Yanga kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikishi kwa kuichapa Azam FC kwa penalti 6-5 katika fainali kali iliyopigwa kwenye Uwanja wa New Amaan visiwani Zanzibar na kwa sasa inasubiriwa tuzo za Wanamichezo Bora, huku kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mudathir Yahya akipewa u-MVP mapema na nyota anaocheza nao Jangwani.

Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) kwa msimu zitafanya wakati wa mchezo wa Ngao ya Jamii tofauti na awali zilipokuwa zinafanyika siku tatu kabla ya kumalizika kwa fainali ya Kombe la Shirikisho, lakini kabla ya tuzo hizo kutolewa, nyota wa Yanga, Khalid Aucho na Kennedy Musonda kwenye ukurasa wa Mudathir Yahya wamemtunuku tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka (MVP).

Kupitia Instagram ya Mudathir aliweka picha akiwa na wawili hao baada ya kuchukua kombe la pili msimu huu baada ya kuchukua la Ligi Kuu na ndipo Aucho aliandika;

"Familia mchezaji wangu bora wa msimu, endelea kufanya kile unachofanya vyema zaidi ya msimu huu." Kwa upande wa Musonda aliandika;

"Familia kwangu umekuwa mchezaji wangu bora na thabiti zaidi msimu huu kaka endelea kupambana."

Mudathir alimaliza msimu na mabao tisa akiwa kwenye 10 bora ya vinara wa mabao wa Ligi Kuu, ambapo Stephane Aziz KI anayekipiga pia katika timu hiyo akibeba kiatu cha dhahabu baada ya kupachika mabaoi 21 katika Ligi Kuu Bara, huku Clement Mzize akibeba kwa upande wa Kombe la Shirikisho akifunga mabao matano akilingana na Edward Songo wa JKT Tanzania inayocheza play-off ya kuepuka kushuka daraja.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: