Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mudathir ni 'mtaala tosha wa elimu' - Oruma

Mudathir Yahya Msd.jpeg Mudathir Yahaya Abbas.

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kutoka EFM, Wilson Oruma amemwagia sifa kiungo wa Yanga, Mudathir Yahya Abbas akisema kuwa mchezaji huyo amekuwa tishio kwa siku za hivi karibuni kutoka na uwezo wake wa kuwasoma mabeki wa wapinzani na kutupia kambani.

Oruma amesema hayo mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa juzi wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa bao 4-0 dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria huku Mudathir akifunga bao la kwanza kabla ya Aziz Ki, Musonda Kennedy na Guede Joseph kuihakikishia Yanga kutinga robo fainali.

"A Third Man Runner King, Mudathir Yahaya Abbas glossary ya soka. The optimal Football litmus test. Kama una appreciate kile ambacho anafanya, unajua Football.

"Ukimtazama Kwa ukaribu Mudathir Yahaya Abbas ni Mtaala.Ni Elimu inapaswa kufundishwa Kwa vijana wote wanaotamani kucheza Football hasa kwenye hii nafasi yake chini ya Miguel Angel Gamondi

"Ni ideal Midfielder kwenye Kila Phases ya Mchezo.Kwenye Kiwango chake ana tick kwenye Kila box muhimu (Physical,Mental and technicall).Lakini pia ni SPECIALIST

"Specialist kwa maana sio wachezaji wengi ni watalaamu kwenye kusoma movement za wapinzani. Muda anajua muda Sahihi Space itafunguka kwenye box la team pinzani.

"Sio wachezaji Wengi wanajua mwisho wa pasi ya 3 baada ya Combination Passes ya wachezaji 2.

"Tayari ana goli 8 msimu huu na Kila goli ni copy and paste ya goli lililopita. CR Belouizdad hii Mechi wanatakiwa kushukuru Mungu imemalizika 4-0 . Ilitakiwa kuwa 5 au 6.

"Note; Guys Kama Gongowazi walishawahi Kukufunga 5 na ukasingizia wachezaji wameuza mechi unatakiwa kuwaomba radhi. Hii football ya Yanga Africa inahitaji nafasi Kwenye Robo Fainali ya CAF champions," amesema Oruma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live