Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mudathir kuikosa Simba Kwa Mkapa?

Rgf Mudathiriiii Mudathir kuikosa Simba Kwa Mkapa?

Wed, 25 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mastaa wawili wa Yanga na Azam FC watarajie rungu la Sh500,000 na kufungiwa mechi tatu kutoka bodi ya ligi kutokana na kitendo walichokifanya kwenye mchezo wa juzi, Jumatatu uliomalizika kwa mwenyeji kuibuka na ushindi, huku presha kubwa ikiwa kwa Yanga ambao wanaweza kumkosa kiungo huyo kwenye mechi yao dhidi ya Simba.

Kwa mujibu wa kanuni ya 41:5 (5.4), kufanya kitendo chochote cha aibu, kama vile kukojoa uwanjani, kukataa kupeana mkono na mgeni rasmi, waamuzi na wachezaji wa timu pinzani, kutoa au kuonyesha ishara inayoashiria matusi ni kosa.

Feisal Salum wa (Azam FC) na Mudathir Yahya wa (Yanga) wamezua taharuki kwa kutegeana kuingia eneo la kuchezea la Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Tukio hilo lilitokea wakati vikosi vya timu hizo vikiingia uwanjani hapo tayari kuanza dakika 45 za kipindi cha kwanza na wachezaji hao walisimama kwenye mstari wa kuingia eneo la kuchezea.

Fei Toto alikuwa anafanya mazoezi ya viungo kwa kunyoosha miguu huku Mudathir akikung’uta viatu vyake ili kuvuta muda wa nani awahi kuingia uwanjani kitendo ambacho bodi ya ligi inatafsiri kama imani za kishirikiana na kutoza faini.

Mastaa hao walikuwa nje kwa muda wakati wachezaji wenzao wakijipanga na kusalimiana, Feisal na Mudathir waliendelea kutegeana hadi zoezi hilo lilipokamilika huku kila kikosi kikienda upande wake.

Wakati taharuki kwa mashabiki ikiwa kubwa baada ya kushtukia kitendo hicho, ndipo Mudathir alipoamua kuwa wa kwanza kwenda kuungana na wenzake huku Feisal naye akifuata na kupiga picha za vikosi.

Msimu uliopita mastaa wa Simba na Yanga Aziz KI na Clatous Chama, walilipishwa faini ya Sh500,000 na kufungiwa kutokucheza mechi tatu za Ligi Kuu Bara zilizokuwa zinafuata kwa kosa kama hilo.

Ilielezwa katika mechi namba 64 ambayo ilizikutanisha Yanga na Simba katika Dimba la Mkapa Oktoba 23, 2022 walikwepa kusalimiana.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, adhabu hiyo ni kwa uzingativu wa kanuni ya 41:5 (5.4) ya ligi kuu udhibiti kwa wachezaji msimu uliopita.

Hii ina maana kama kamati itakaa mapema Fei na Mudathir wanaweza kukosa michezo mitatu ijayo, Yanga mechi zao ni dhidi ya Singida, Simba na Coastal Union, huku Azam wakiwa wanasubiri kucheza na Namungo, Mashujaa na Ihefu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: