Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mudathir asiachwe kwenye kinyang'anyiro cha kiungo bora

Mudathir  16.jpeg Mudathir asiachwe kwenye kinyang'anyiro cha kiungo bora

Tue, 21 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nipo kwenye social media ninaona mijadala kuhusu nominees mbalimbali wa tuzo za msimu 2023|24 za ligi kuu Tanzania bara.

Kuhusu tuzo ya kiungo bora wengi wanayataja majina yafuatayo :

◉ Stephane Aziz Ki.

◉ Feisal Salum.

◉ Khalid Aucho

◉ Marouf Tchakei.

Naomba niwaongezee jina moja :

◉ Mudathir Yahya.

Kwa nini Mudathir Yahya Abbas?

Miongoni mwa wachezaji wa Yanga SC aliyepatikana muda mwingi kiwanjani kwa consistency ileile mwanzo wa msimu hadi mwisho, aliyevuja jasho jingi kuipigania timu yake hadi kutwaa Ubingwa wa ligi kuu 23 | 24 huwezi kumuacha Mudathir Yahya.

Mpaka sasa ligi kuu Tanzania bara sikumbuki ni lini KIUNGO WA CHINI aliyefunga magoli mengi (9) ligi kuu kumzidi Mudathir, naomba nikumbushwe.

Mudathir ana mabao (9) na Assists (4) ligi kuu mpaka sasa. Katimiza jukumu lake mama la KUKABA lakini pia katoa BONUS ya kuhusika katika mabao (13) ligi kuu.

Sawa, Aziz na Feisal wamefunga magoli mengi kumzidi ndio, lakini ukitazama role wanazocheza utaona kabisa magoli (9) kwa kiungo wa CHINI ni mengi mno, tena ukizingatia Feisal na Aziz hasa Fei anatajwa kama kiungo lakini ukitazama mechi nyingi anacheza kama forward msimu huu.

Mpaka Yanga wanatwaa Ubingwa, Mudathir Yahya ni miongoni mwa wachezaji top two kwenye ligi nzima aliye score points nyingi zaidi katika magoli yake aliyofunga.

Magoli mengi yalikuwa ya kuamua mechi, takribani mechi (5) za Yanga msimu huu ambazo Yanga alikuwa anaenda kusare sawa na Points (15) Mudathir alihakikisha points zote (3) za kila Mchezo zinaenda jangwani.

Mudathir ndiye mchezaji aliyeipa points nyingi zaidi Yanga katika dakika za mwisho kuliko mchezaji yoyote msimu huu.

⚽ Mudathir - (88') vs Namungo (1-0)

⚽ Mudathir - (87) vs Dodoma Jiji (1-0)

⚽ Mudathir - (85') vs Mashujaa (2-1)

⚽ Mudathir - (82') vs Kagera sugar (1-0)

Wengi ni kama wanachukulia poa alichokifanya msimu huu pengine labda kwa kuwa ni mzawa lakini kwangu ana kila sifa ya kuwania tuzo ya kiungo bora.

Wote hapo juu wanastahili tuzo, ikitokea Mudathir kakosa tuzo basi hata akiwekwa katika NOMINEES tu INATOSHA kuonesha wametambua mchango wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live