Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mudathir amtaja rasmi anayempigiaga simu

Mudathir Yahya Msd.jpeg Mudathir amtaja rasmi anayempigiaga simu

Wed, 15 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Yanga, Mudathir Yahya Abbas amefunguka kuhusu staili yake ya kushangilia kwa kupiga simu ambayo imekuwa gumzo hasa tangu ajiunge na Yanga.

Awali ilikuwa inadaiwa kuwa, Mudathir anampigia simu Fei Toto ambaye aliondoka yanga kwenda Azam FC huku akimtaja mtu ambaye amekuwa akimpigia simu.

Msikie Mudathir; “Simu yangu huwa inakwenda kwa mwanangu na mke wangu kwa sababu mwanangu ni mdogo lakini anapenda sana simu, ningekuwa na simu hapa ningekuonesha mtoto mdogo lakini anapenda mambo ya simu.

“Huu ni msimu bora kwangu kwa kufunga na kutengeneza nafasi, mechi kama hii nimetengeneza nafasi mbili wenzangu wakafunga na tumefanikiwa kutwaa ubingwa kwa mara nyingine tena, ni jambo kumshukuru Mungu,” amesema Mudathir.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live